Safari Yetu Ya Kufana
Nilikuwa nikilala fofofo, mara tu kwa ghafla nikaskikia jimbi akiwika kwa maringo akijaribu kutuamsha kutoka usingizini. Nilipofungua macho yangu, niliuona mwangaza ukipenya chumbani mwangu.
Niliamka na kudemka demdem huku nikielekea dirishani kufungua pazia. Nilimuona mfalme wa mwangaza jua akipaa huku akirusha miale yake mikali huku na huko.
Nayo maua yalikuwa yakifunguka kwa ishara ya kukaribisha siku. Chini, niliona kuking’ara kama almasi kwenye jua kwa sababu ya umande uliomulikwa na jua. Nao ndege waliruka huku na kule wakiimba nyimbo zao za kifahari.
...