Elimu ni ufunguo wa maendeleo ya Afrika lakini katika maeneo kadhaa shule na vyuo vikuu bado ni vichache. "Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako" kinaleta elimu katika kila eneo la bara hilo.
Maisha yanabadilika kwa haraka katika bara la Afrika: Mtandao wa Internet pamoja na matumizi ya simu za mkononi yanazidi kukua, lakini maelfu ya watu bado wametengwa na dunia ya vyombo vya mawasiliano. Vijana wa Kiafrika wanatafuta nafasi yao katika jamii ya dunia ambayo imejikita katika elimu na wanawaza ni njia gani itawafikisha katika kazi bora ama elimu bora. Kwa mfano, wengi wanajiuliza ni nafasi gani za elimu na mafunzo zinapatikana katika mtandao na ni nafasi gani utandawazi unaweza kusaidia. Maelfu kwa maelfu wanataka kwenda kupata elimu katika bara la Ulaya, lakini hawafahamu kile kitakachotokea huko waendako.
Thank you very much!!